X hits on this document

PDF document

Uvumbuzi wa Isimu Amali - kwa Wajaluo, Kenya - page 1 / 9

70 views

0 shares

0 downloads

0 comments

1 / 9

Isimu amali kwa Wajaluo

Uvumbuzi wa Isimu Amali - kwa Wajaluo, Kenya

uhusiano wa lugha na utamaduni wake

Maandishi haya yameandikwa na: Jim Harries (Kima International School of Theology,

PO Box 75, Maseno, Kenya. jimoharries@gmail.com

tel. 0734 923403) ili

yasomwe katika chuo cha Maseno, Institute of Research and Post-Graduate Studies.

Jim Harries (anayeitwa pia Jacob Otieno akiwa nyumbani) ni mmisionari chini ya Church of God, Kenya. Anafundisha katika Shule ya Biblia ya Church of God Kima, na pia kwa Yala Theological Centre, Yala, Gem. Pia ni mwanafunzi wa PhD, Birmingham University, UK,

Tarehe ya uchapishaji: 16.06.04

Nilipoishi Zambia miaka 1988 mpaka 1991, nilishangazwa kwa matumizi ya Wazambia ya lugha ya Kiingereza. Mara nyingi maneno walioyatumia hayakutosha kunifahamisha maana ambayo walilenga. Nilijiuliza, hilo ni jambo gani? Je, Wazambia ni wabaya ambao hawapendi kuongea ili waweze kueleweka au ni mimi ambaye sijafahamu mambo yao? Niligundua kwamba lazima kosa lilikuwa langu. Lazima nijitolee ili niwaelewe.

Bada ya kuondoka nchini Zambia, kuanzia 1993 mpaka sasa nimekuwa nikiishi Yala, Gem, kwa Wajaluo wa Kenya. Ninaishi kijijini nikifanya kazi ya kanisa. Tunao mpango wa mafunzo ya Biblia hapo Yala. Pia ninafundisha katika chuo cha Kima International School of Theology, Bunyore, chini ya Church of God.

Pamoja na kufundisha Biblia nimejitolea ili nijifunze Kiswahili na Dholuo. Mambo mengi ambayo ninayataja kuwahusu Wajaluo na lugha yao haimaanishi kwamba yanahusika na Dholuo peke yake, ila Dholuo ni lugha ambayo nimeweza kujifunza kwa undani kiasi fulani. Hapo nimepata changamoto kubwa sana. Ninawashukuru watu ambao wamenisaidia kujifunza lugha zao, na pia kwa kiasi fulani mila na desturi zao. Kwa makosa yeyote yanoyojitokeza sasa, simlaumu ye yote ila ni yangu tu.

Mnamo mwaka wa karibuni utafiti wangu ulinifanya nichunguze semantiksi, ili nijisaidie kufahamu juu ya lugha na maana yake. Nilistaajabu nilivyo soma maandishi ya Kempson juu ya nadharia ya semantiksi (1977): "...there is almost no aspect of semantics with which there is any degree of certainty" (p184) anaandika Kempson. (Hatuwezi kuwa na uhakika na karibu mambo yoyote kwa somo la semantiksi). Njia ya kugundua maana ya sentensi ni kusema "S is true only if P" (23), S ikiwa sentensi, na P ikiwa sharti linalouhakikisha ukweli wa sentensi. Kwa hivyo tunaweza kusema "majani ni mabichi (S) ikiwa majani ni mabichi (P)." Niligundua kumbe kuchunguza semantiksi haitakuwa na msaada sana kuniwezesha kukamilisha lengo langu la kuwafahamu Waafrika ili kazi yangu ya kufundisha Biblia iwe ya maana. Lakini, Kempson anatuelekeza kwa isimu amali (pragmatic linguistics) au 'matumizi ya lugha' (Kempson 1977:47).

Nilianza kugundua kwamba maana ya lugha inatokea kufuatana na utumiaji wake! Jinsi lugha inavyotumiwa, na mahali au muktadha wake unachukua sehemu kubwa kuhusu uvumbuzi wa maana. Nilijichorea ifuatavyo:

Fonetika---> syntaksi---> semantiksi---->amali

1

Document info
Document views70
Page views71
Page last viewedMon Jan 23 15:19:35 UTC 2017
Pages9
Paragraphs145
Words4238

Comments