X hits on this document

PDF document

Uvumbuzi wa Isimu Amali - kwa Wajaluo, Kenya - page 2 / 9

63 views

0 shares

0 downloads

0 comments

2 / 9

Isimu amali kwa Wajaluo (phonetics)--->(syntax)--->(semantics)--->(pragmatics)

Uvumbuzi wa maana ya utamshi fulani unategemea kwa kiasi kubwa sana eneo na muktadha wake. Sasa, muktadha unapobadilisha, je maana yanakosakufahamika? Hapo ndipo panaweza kuwa mwanzo wa jibu la swali kubwa langu!

Ni Grice ambaye anakubaliwa kuwa moja wa waanzilishi wa mijadala juu ya amali ya lugha (Levinson 1983:16). Grice aliunda nadharia ya cooperative principle - sheria ya msingi inayofuatwa ili watu wawasiliane barabara. Aliunda sheria yake kwa sehemu nne:

 • 1.

  (Quantity) - mtu ataeleza mambo ya kutosha na sio zaidi.

 • 2.

  (Quality) - mtu ataongea kitu cha kweli.

 • 3.

  (Relation) - anachoongea mtu kitahusisha wasikilizaji.

 • 4.

  (Manner) - jambo litajadiliwe kwa uwasi.

Leech (1983) alianza kupinga msingi uliowekwa na Grice. Sisi leo tutamfuata sana Leech, sababu anaeleweka wasi kwa jinsi anagawa mambo ya Grice kwa masehemu.

Lengo langu ni kuonyesha jinsi matumizi ya Wajaluo kwa lugha yao (Dholuo) haufuatani na sheria za Grice, na vile hali hio inafanya kusikilizana kati ya Wajaluo na wenye asili cha Kiingereza lazima kuwe ngumu.

Mjaluo anaishi kwa dunia pamoja na wafu (juogi / jochiende). Kwa ufahamu wake, hawa wafu (mizimu) wanaweza kuwa wana sikiliza mijadala yo yote inayoendelea. Kwa hivyo mjadala unaonekana kuwa kati ya watu wawili (yaani dialogue) unasikilizwa na watu wengi (yaani polylogue; Kerbrat 2004). Swali ambalo wengine wanaweza kuuliza "are the spirits real" ni duni. Mjaluo anajua wapo. Pia, wengi wao hupenda kuleta uovu. (Shuguli ya mjaluo pande ya juogi na jochiende, zaidi sikuhizi, ni kujikinga nao. Maana yake, wanaonekana kuwa waovu.) Uzuri sasa unafahamika unatoka kwa Nyasaye (Mungu) na maisha ya kisasa.

Egner alishangaa kwa matumizi ya lugha ya watu wa Ivory Coast (Egner 2002). Anaeleza jinsi mtu mmoja alimwaahidi atakuwa naye kwa sherehe fulani, lakini pia siku ile alikuwa amepanga kuwa kwa mji mwingine mbali na hapo. Ni kama ahadi yake ilikuwa bure kabisa. Egner anajaribu kueleza jinsi kufanya ahadi kwa Waafrika maneno lazima yarudiwa maradufu (Egner 2002). Lakini Mhogolo anatuambia "kwa ... mtu mgeni, mtu (Mwafrika) akaweza akamwambia vingine ambavyo si kweli ama uongo" (1985:64). Kwa hivyo, matumizi ya lugha kwa Mwafrika sio lazima utaje ukweli kwa mgeni. Mwafrika pia hapendi kumwambia mtu 'la' uso kwa uso. Afadhali aseme 'ndio', hata ikiwa anajua atashindwa kutekeleza jambo hilo. Kukataa katakata maneno yanayo ongolewa kwa lengo nzuri ni kukosa heshima. Kwa njia ingine tena tunaweza sema abiro biro ('nita kuja') kwa Dholuo inafaa itafsiriwe kwa Kiingereza kuwa 'I would like to come' na sio 'I will come'.

Wengine wanaweza kusema, Wajaluo siku hizi wameshawachanana na imani yao ya awali ya jochiende na juogi. Hata ikiwa hivyo, lazima tuendelee kujiuliza ikiwa njia ya matumizi wa lugha unaweza kubadilisha mara moja watu wakisema wamewachana na ushirikina? (Mara nyingi ninasikia Mwafrika mweusi hawezi kuwachana na imani yake kwa nguvu ya mizimu, lakini sasa tuseme hata ikiwezekana). Je, mazoezi ya matumizi wa lugha haitaendelea? Ni rahisi mtu kusema 'simwogopi simba', lakini akijikuta anavamiwa na simba, je hatakimbia? Hivyo ndivyo wale wanaokataa imani kwa Mungu wakiwa mahututini. Hivyo ndivyo wanaokataa hawaamini kwa uwezo wa Wafu.

2

Document info
Document views63
Page views64
Page last viewedTue Jan 17 03:19:27 UTC 2017
Pages9
Paragraphs145
Words4238

Comments