X hits on this document

PDF document

Uvumbuzi wa Isimu Amali - kwa Wajaluo, Kenya - page 3 / 9

64 views

0 shares

0 downloads

0 comments

3 / 9

Isimu amali kwa Wajaluo

Mtu moja akibadilisha hali yake kuongea, mara moja hatafahamikwa na wenzake. Kwa hivyo uzoezi wake utaendelea kumwongoza. Kwa hivyo, kubadilisha kwa hali ya eneo na imani (dini) ya Mjaluo haitaleta mabadiliko kwa matumizi wa lugha yake mara moja.

Nilipokuwa ninatembea kwa barabara ya Maseno-Kisumu kabla haija tengenezwa juzi, niliweza kushangaa gari inapokuja kutoka mbele vile mara moja inageuka na kutuelekea kamili kwa kufuata pande yetu ya barabara. Tulipofika hapo mahali pa kisa hiki, shimo kubwa barabarani ilionekana wazi. Hivyo ndivyo mtu anaweza kuitumia lugha kwa njia ya kutofahamika kwa mtu ambaye hajaona shimo, yaani mzimu.

Mbali na CP (co-operative principle), ni rahisi kwa Mjaluo kusema kitu ambacho sio 'kweli'. Hivyo atakuwa anatumia lugha ili ajihepe na uovu fulani unao mwelekea. Mifano, ipo kueleza hali hiyo kwa kitamaduni ya Wajaluo. Kwa mfano, inasemekana Mzee Mjaluo anajaribu kutumia njia tofauti kila siku kutoka na kurudi nyumbani (Mboya 1978:np). Anafanya hivyo ili mtu asimwekee dawa njiani mwake ambayo itamuumiza. Tena mwanamke mwenye kisoni (watoto wake wana kufa wakiwa bado wadogo) anaponywa kwa kumdanganya pepo wenye kifo ili atambue mtoto ameshaaga - halafu amwache bila kumsumbua. Pepo anadanganywa kwa kumpelekea mtoto msituni na kumwacha hapo kwa muda kidogo, mtu akipiga sauti ya fisi. Hivyo pepo wa kifo anaenda kwake na anamwacha mtoto aishi. Kwa hivyo Mjaluo anatumia lugha kumdanganya pepo (km jachien), maneno yakiwa kweli au la. Tena hivyo mazingira ya mtu yanatengenezwa kupitia kwa matumizi ya lugha! (Ifahamikwe hapa lugha ni chombo cha uundaji na sio uelezo peke - Steiner 1998:275).

Kwa hivyo Mjaluo anafahamu amepewa lugha yake ili aitumie kujikinga na uovu - bila kujali ikiwa anachosema ni kweli au la.

Austin alikiita kitabu chake Doing Things with Words (1962). Anaeleza humo jinsi maneno mengi yanatumiwa sio kueleza kitu bali kufanya kitu, Mambo ambayo Wajaluo wamekuwa wameyafahamu tayari kwa miaka mingi. Maneno yanaweza kutumiwa kuwadanganya au kuwafurahisha mizimu kwa faida ya mtu mwenyewe.

Leech anatuambia kufuatana na CP watu huongea na informativeness required (kuyaeleza mambo kwa kiasi yanavyohitajikwa). Hapa tunaweza kujiuliza, yanayohitajika ni yapi? Leech anafahamu 'yanayohitajikwa' ni kulingana na ufahamu wa dunia ambayo yanakuwa haina watawala wengine kama miungu au mizimu, ila watu tu. Tena watu ambao wanalenga kusaidiana. Mambo ambayo yapo tofauti kwetu hapo Luoni.

Nikiwa Luoni, ninavyo mwambia mtu niliona ng'ombe wake sio mzima, atajiuliza kwa nini nimekuwa nimewaangalia ng'ombe wake? Pengine kumbe ni mimi ndiye nimewaroga ng'ombe wake, na sasa ninafurahia kwa balaa yake. Nikiuliza tena ikiwa amefaulu kuwalipia watoto wake karo ya shule, nisipokuwa na pesa kumpa atafikiria ninauliza kwa lengo mbaya. Kwa ujumla tunaweza sema mambo mengi ya maisha ya mtu hayapo wazi kujadiliwa na mtu mwingine asipokuwa mhusika mwenyewe. Hatua moja tu baada ya kuyaficha mambo tuna kuja kwa kutaja uongo juu ya mambo. Kila mtu hana pesa au mali, sababu anaogopa akikubali kukuwa nayo yakutosha atarogwa na mwenye wivu.

Watu wengi hawaoni kama ni kosa kuyatumia maneno kuunda hali ambayo ni sawa, na sio kuelezea hali vile ilivyo. Mvulana ambaye anataka kuoa kusema ‘hawa ng'ombe ni wangu’, na hata kumwambia mchumba wake anavyo viti, vitanda, pasia na makabati kwa nyumba yake, hahesabiwi mwenye makosa sababu kumbe kitu anachotaka ni kitu kizuri - kumposa msichana. Ni kawaida kwa mtu kujifanya aonekane mtu mzuri na sio mbaya mbele ya watu. Hivyo ndivyo kwa shule yetu ya kitheologia hapo Yala karibu kila mara

3

Document info
Document views64
Page views65
Page last viewedTue Jan 17 19:42:05 UTC 2017
Pages9
Paragraphs145
Words4238

Comments