X hits on this document

PDF document

Uvumbuzi wa Isimu Amali - kwa Wajaluo, Kenya - page 4 / 9

68 views

0 shares

0 downloads

0 comments

4 / 9

Isimu amali kwa Wajaluo

tukimwongelesha mtu anasema atakuja kuhudhuria mafunzo yetu, halafu haonekani. Kwa kuongea kwake amejifanya aonekane mtu sawa. Amejiokoa kwa hali duni ambayo inataka kumshinda na hajali sana kuwa amevunja CP (cooperative principle)!

Tuko mbali na Leech, anayetuambia mtu hatasema kitu bila uthibitisho au uhakika fulani juu ya ukweli wa neno lake. Mara nyingi nimejikuta ninasubiri kitu, kwa mfano basi kufika au stima ambayo imepotea kurudi. Mtu akiniona ninayo wasiwasi, au nikimuuliza mwenzangu atasema 'basi inakuja saa hii' au 'stima iko karibu kurudi'. Kwa ukweli hajui, lakini anapenda kunihimiza kuliko kukubali ujinga wake na kuniwacha kwa wasiwasi.

Uponyaji tena ni hivyo. Baada ya kumwombea mtu, haifai kusema hali yake bado haijabadilika. Hapana. Unahitajika kusema 'sasa amepona', ili maneno yetu yamsaidie huyu mtu ili kweli apone.

Omari (1993) anakubali katakata na hali ya ushirikina wa Watanzania. Iteyo anagundua

jamaa ya waafrika wanakubalia kuwepo kwa mapepo

(“incorporeal things

2002:150). Ni matokeo ya imani aina hiyo panda ya matumizi ya lugha ambayo ni ngumu

kwa mtu kutoka nchi za Ulaya kutambua au kufahamu. Makosa yake mara nyingi ni kutotambua uhusiano wa imani ya ushirikina na jinsi mtu anavyotumia lugha yake.

CP pia inatuambia mtu ata avoid obscurity of expression. Je, hii ni sawa kwa bara la Afrika? Amuka (1978) hangeweza kukubali, kwa vile anafafanua njia ya Wajaluo kuongea kupitia kwa ngeche (mithali, fumbo au kitendawili). Inaonekana matumizi ya ngero unamfurajisha mtu. Hivyo kitu au hali ambayo ilikuwa ya kawaida inachochewa kuwa ya ajabu, ya fumbo, ya kuchekelewa. Maneno yanatumiwa hivyo kuunda hali ingine juu ya hiyo ambayo inaonekana na macho. Kumwambia mtu mi mana pieri (kaza matako yako) ili umhimize afanye bidii ni kumwongeza hali ya uchanga moto pamoja na furaha moyoni, kupitia kwa obscurity (fumbo) mwenyewe!

Kupinga maneno ya Grice na Leech, Sperber na Wilson (nd) wameunda nadharia nyingine ya relevance, yaani uhusiko. Wanasema mtu atayafahamu maneno au utamshi kwa kutumia maximum cognitive effect and minimum processing effort, yaani wingi wa uhusiano na mawazo ya mtu kupitia kwa ukazo ya ubongo kidogo. Tuseme, maana ya utamshi unaosikika utatambuliwa kwa njia hizo, zinazohusiana na hali ya mtu. Nikiambiwa 'ameenda' nikijua daktari wa ng'ombe yuko nitajua huyu ng'ombe aliyekuwa mgonjwa ameaga dunia. Nikiambiwa hivyo baada ya kumsubiri mtu kumsindikiza mtoto wangu shuleni nitajua ni mtoto wangu ambaye ameenda (shuleni).

Sperber na Wilson wanawaandikia watu Waulaya , ambao wanaonekana hawana uhusiano na mizimu / mapepo maishani mwao. Wakielezwa juu ya mambo fulani hali ya uhusiano mawazoni mwao itawaelekeza kisiensi. Kwa mfano, wakiambiwa 'kiti kimevunjika' wanaweza kufikiri 'kumbe chuma kilichotumiwa hakikukuwa kimetengenezwa na nguvu ya kutosha'. Lakini mtu wa bara la Afrika kuambiwa hivyo atajiuliza ni nani aliye sababisha kitendo hicho? Tukiendelea kutafakari juu ya hayo tutagundua kwa kutafuta hali ya uhusiano wenye maana mahali Mgaribi atakapoona siensi, Mwafrika hataiona! Inapotea kwa maandiko!

Hio inatuonyesha vile maandiko ya kisiensi yataweza kufahamikwa kwa Mwaafrika kama yawe ya ushirikina, na hali kadhalika maneno yaliyoandikwa juu ya ushirikina na Mwaafrika yatafahamika kwa mtu wa Ulaya kama maneno ya siensi! Amali ya maneno yanayageuza maana yao kabisa! Kiini cha maandiko kinaweza kupotea chupu chupu.

4

Document info
Document views68
Page views69
Page last viewedSun Jan 22 22:18:34 UTC 2017
Pages9
Paragraphs145
Words4238

Comments