X hits on this document

PDF document

Uvumbuzi wa Isimu Amali - kwa Wajaluo, Kenya - page 5 / 9

69 views

0 shares

0 downloads

0 comments

5 / 9

Isimu amali kwa Wajaluo

Nadharia inachosema maneno yanatumiwa kukifanya kitu na sio kueleza juu ya kitu, kinahitajika kuchunguzwa zaidi. Austin (Kempson 1977:51) anatuambia kila tamshi la mtu linalo mambo ya locutionary, illocutionary na perlocutory. Kitendo cha locutionary, kina kuwa maneno yenyewe. Kitendo cha illocutionary kwa hilo tamko kinakuwa nguvu fulani, ikiwa kusifu, kulaani, kupinga nk. Kitendo cha perlocutionary ni matokeo yanayotakikana kwa msikilizaji, ikiwa kutahadhari, kutengeneza chai, kucheka nk. Itafahamika kwamba l o c u t i o n f u l a n i i n a w e z a k u w a n a i l l o c u t i o n n a p e r l o c u t i o n m b a l i m b a l i , k u l i n g a n a n a 'Nimekuona' linaweza kuwa ya maana 'asante kwa kujifichua', linaweza mazingira.

kuwa onyo ili usiibe, au furaha sababu nimekuwa kipofu kwa muda mrefu! Kulitaja hilo neno linaweza kukufanya ujitokeze zaidi, uregea mikono yako mfukoni mwako, au uanze kushangilia nami pamoja.

Uchunguzi bado unahitajika hapo, lakini ninatumaini tumetambua uhusiano kubwa sana hapa wa maneno na mazingira au hali ya matumizi yao.

Kuna neno kwa Kiingereza la politeness. Neno linalo weza kwa Dholuo kulinganishwa nalo pengine ni luor, lakini ufananishi ninaoona haupo sana. ('Mos' au 'muol' yanazeza kutafsiri 'polite', lakini tena yapo mbali kiasi.)

Ila, neno hili la politeness, linaonekana lina umuhimu sana kwa Kiingereza, mpaka vitabu vimeandikwa juu yake, kwa mfano katibu cha Brown na Levinson, (1987). Hawa husema " the most subtle differences in ... pragmatic features of a linguistic variety are sufficient to engender mismatches in perceived politeness." Yaani utofauti kidogo kwa isimu amali unaweza leta hali ya kutoongea na heshima (politeness) ambayo inatarajiwa. Lakini lengo la politeness ni kupunguza hali ya kuonekana mwenye ukatili. Maana yake, mtu asiyefahamu matumizi ya lugha yenye politeness (luor / heshima) hatawezakujenga uhusiano mzuri na watu, ambao watamdhania mkatili.

Mijadala imekuwa mingi juu ya luor au heshima. Mimi ninataka kusema msingi wake kwa sisi Luoni ni uoga wa vitendo vya wafu wakijisikia wanakosewa. Hali hiyo inayomsingi tofauti sana na hiyo ya politeness ya Kiingereza. Maana yake, mambo ya kujifunza aina ya politeness / luor (heshima) kwa mwenye Kiingereza akitaka kujua Dholuo (au lugha zingine za Afrika), au Mjaluo kujifunza ili afahamu matumizi ya Kiingereza ni nyingi sana, na yaumuhimu sana, na ambayo hayafunzwi shuleni. Pasipo hayo, uhusiano wa karibu ambao unahitajika (kwa mfano) ili kufanya kazi pamoja, haumo.

Je, tunataka kujaribu kuwafunza watu politeness kwa matumizi ya Kiingereza, ambayo ni lazima tukitaka kuwasiliana kwa karibu na Wazungu kutoka nchi za nje? Au, tuendelee kufunza Kiingereza ambacho hakitaweza kuleta uhusiano? Au tufanyaje kwa hayo?

Karibu na politeness ni face-saving. Ninavyoona mwenyewe tena, haupo sana kwa Wajaluo wala Waafrika. Kwa mfano, nikihitaji kuenda shuleni, na mvua inanyesha na wewe una gari, Kiingereza kinachotumiwa kwa Ulaya kina weza kuwa "you wouldn't mind giving me a lift would you?" (je, hungeweza kutojali kunipa ubebaji au?) ili mtu asiaibishwe akikataa. Lakini ninavyo sikia utumiza wa lugha kwa Kenya inakuwa "give me a lift" (beba mimi). Lakini sheria za luoro kwa Waulaya hawajui. Wanaweza kumwita mzee mheshimiwa "Bob" badala ya "Mzee" (Sir), mwalimu 'hi mate' nk.

Ogot anajadiliana sana juu ya hali ya usawa na hali tena ya utofauti kati ya Waafrika na watu wa Ulaya (Ogot 1999:79-88). Ogot anamaliza akisema hakuna kitu kama hali ya kipekee ya mawazo ya Mwaafrika.

5

Document info
Document views69
Page views70
Page last viewedMon Jan 23 10:47:59 UTC 2017
Pages9
Paragraphs145
Words4238

Comments