X hits on this document

PDF document

Uvumbuzi wa Isimu Amali - kwa Wajaluo, Kenya - page 6 / 9

67 views

0 shares

0 downloads

0 comments

6 / 9

Isimu amali kwa Wajaluo

Bila kukosa kumheshimu Ogot, pengine kitu ambacho hakukitambua ni wenye mawazo ya kipekee sio Waafrika, ila Wazungu wa Ulaya wa magharibi! Historia inatuonyesha vile walipitia kwa mambo mengi kama ya enlightenment na age of reason (kwa mfano angalia Cragg, 1960) ambayo imewapa mawazo tofauti na watu wengine wote duniani mzima na kwa historia yote. Wanaolenga kuwaiga au kuwafahamu hawa watu (Wazungu) wanajitakia kazi ngumu mno. Hata Waafro-america wameshindwa kiasi kubwa kufanya hivyo, na wanaishi kwa nchi ya magharibi kama raia! Afadali kujiheshimu mwenyewe, kujifunza kwa wengine, lakini sio kujaribu kukuwa kama hao - kitu ambacho hakitawezakuwa rahisi. Kila watu ni tofauti, na mambo yanayowafanye vile walivyo ni mengi na aina ya kushindwa kufahamishwa.

Kusikiliza wakati wakalimani wanafanya kazi yao kinaweza kumfaidi mtu sana. Ninavyowasikiliza wenye kutafsiri Dholuo mpaka Kiswahili, ninaweza kushangaa. Kwa kweli maneno kadhaa ya Dholuo hayawezi kutafsiriwa kata kata. Badala yake jachien mar homa inakuwa tu 'homa', chike mag dala inakuwa 'mambo', dala doho inakuwa boma kubwa nk.

Ukweli wa mambo ni ukalimani unapoteza mambo mengi. Kwa njia ingine ukalimani ni uundaji, wa kitu kipya kabisa. Maana asili yakitafsiriwa na kusikilizwa na watu ambao hawaifahamu mila ya asili, yanapotea. Badala yake wanasikia juu ya 'wageni ' hawa kama kundi la watu wao wenye hali ya juu wa ujinga! Wenye lugha na mila ya Kiingereza wakisikia ukalimani wa Dholuo wataweza tu kuwagundua Wajaluo wakiwa aina ya watu wao. Hivyo ndivyo tena kwa Mjluo akiwasikiliza juu ya watu wa Ulaya.

Sababu za hiyo kutokea ni nyingi, zingine ambazo zimeelezwa hapo juu. Mimi ninavyoona, kwa kiasi kubwa Mwingereza hawezi kumfahamu Mjaluo, na hivyo tena Mjaluo Mwingereza - kupitia kwa lugha peke yake! Kutoweza kumfahamu, maana yake ni kutomfahamu au kumfahamu kwa njia bure au mbaya. Ili uwafahamu watu lazima uishi nao! Waafrika (Wajaluo) wameunda mawazoni mwao vile wanafikiri juu ya Wazungu, ambao sio kikamilifu, na huo uundaji ambao haupo, ndio wanajaribu kuiga!

Ukalimani unawezekana tu kwa kiwango ambacho mila za lugha zote zinakuwa sawa. Pasipo hiyo - kiasi kikubwa ni uundaji.

Mimi mwenyewe nimekitafsiri kitabu cha Paul Mboya cha Luo Kitgi gi Timbegi (Wajaluo na Mila na Kitamaduni Chao) (1983). Baadaye nikagundua - Waingereza watakao soma utafsiri wangu hawataweza kufurahi na vitendo vya Wajaluo, jinsi msomaji Mjaluo anayeweza kufurahi. Ili kitabu kiwafurahishe Waingereza hivyo kinafaa kiandikwe juu ya "mila na desturi ya Waingereza!" Hii ni hali ya ukalimani ambayo unawezafaa!

Mfano wa ukalimani mbaya kwa mambo ya kanisa ni huo unayoitwa kwa Kingereza prosperity gospel. Kuyatafsiri haya maneno kwa lugha za Kiafrika ni ngumu au hata hakiwezekani. Tukijaribu tunawezapata injili ya maendeleo, au injili ya ufanisi au injili ya mali ya dunia, ambayo inasikika tofauti sana kwa hiyo ya Kiingereza na kwa urahisi inapendeza!

Kwa hivyo ukweli wa mambo ni, utafsiri mbali mbali huthibitisha mambo ya uundaji ambao sio wa kweli, yaani inventions! Mkalimani anayefaa ni huyo ambaye ameshaishi na kuonja maisha ya ndani pande zote. Yaani, Mwafrika ambaye ameishi na Wazungu kwao au Mzungu aliyeishi kwa urefu na Waafrika kwao. Kawaida Waafrika wakienda Ulaya huishi shuleni, au na Waafrika wenzao, na Mzungu akija Afrika hivyo tena; anaishi na Wazungu wenzake mjini au kwa mission station. Anayeweza kufahamu pande zote mbili

6

Document info
Document views67
Page views68
Page last viewedSat Jan 21 14:51:36 UTC 2017
Pages9
Paragraphs145
Words4238

Comments