X hits on this document

PDF document

Uvumbuzi wa Isimu Amali - kwa Wajaluo, Kenya - page 7 / 9

65 views

0 shares

0 downloads

0 comments

7 / 9

Isimu amali kwa Wajaluo

pia anayekazi ngumu zaidi, ambaye pengine hata itamshinda kutekeleza: kuwathibitishia watu juu ya kitu ambacho hawaoni na macho (ya nje au ndani) yao sio rahisi.

Kwa hivyo kwa hali tunayo sasa, ukalimani unadumisha ujinga mwingi.

Nikiongea juu ya ukalimani wenye ujinga, ninamaana pia Mwafrika anayesoma Kiingereza, au Mwingereza anayeweza kusoma lugha ya kiafrika, ambaye hajaweza kujiingiza kwa ndani kwa mila yao. Tuchukuwe mfano wa Mjaluo anayesoma Kiingereza. Kabla hajajifunza (kupitia kwa mazoezi na siyo darasani ambayo hayawezekani) hali ya maisha mengine, lazima atafsiri kila kitu anachosoma kulingana na mila na kitamaduni chake. Atawezaje kufahamu kumbe kunakuwepo kitu kingine tofauti na hiki ambacho amekizoea, isipokuwa kina kuwa cha kukosa hekima? Akikubali uzuri wake, anakubali hali ya kujigonga kichwani kila mara kukubali kitu ambacho moyo wake utaendelea kumwambia ni bure.

Kufikiri inakuwa kupitia kwa kujifunza lugha darasani mtu ataweza kuifahamu lugha kutoka mila ya ugeni kabisa, ni kujidanganya kwa hali ya juu. Kuifahamu lugha bila kujua juu ya matumizi yake ni kujifunza tena lugha ya tatu ambayo sio yako, sio ya mgeni, lakini ingine tofauti tena na ya kipekee. Tuseme ni sheng au pidgin ambayo kuisikia ungefikiri ni Kiingereza.

Nadharia ya Whorf (Sapir-Whorf hypothesis) imechunguzwa sana na wanaisimu (angalia Anon:nd). Je, lugha inamwundia mtu ufahamu wake wa dunia? Mjaluo ambaye hana neno kulitafsiri challenge (changa moto), je, hana changa moto? Mwingereza ambaye hana neno okola ni sababu sio lazima kuridhiwa kwa wajane wake?

Sina nafasi kuchunguza hayo maswali kwa ndani wakati huu. Ila ninaweza sema bila shaka Mwingereza ambaye anajifunza Dholuo anaingiza hali ya mila, kitamaduni na lugha zake kwa ufahamu wake wa Dholuo, na kadhalika Mjaluo anayejifunza Kiingereza. Kujifunza lugha haiwezi mara moja kubadilisha ufahamu wa mtu kwa dunia na binadamu (worldview), kwa hivyo strong Whorfianism (ushikishaji kwa nadharia ya Whorf sana) ninaona haiwezekani. Tena, mtu anaweza kuongea Kiingereza na sarufi yake safi sana, na bado kuwa mjinga kwa mila na kitamaduni cha Waingereza. Hivyo ndivyo kwa Kijaluo pia, ila sio rahisi kujifunza Kijaluo bila kuishi na Wajaluo na hivyo pia kuanza kuifahamu mila yao.

Maneno mawili yanaweza kuwa na maana sawa, lakini bado uzani ya haya maneno yanaweza kuwa tofauti. 'Min David' (mama wa David) na 'min Elizabeth' (mama wa Elizabeth) ni mtu moja mwenye watoto wawili. Kwa ukalimani atawezaitwa pengine 'Mildred', jina ambalo halielezi yoyote juu ya watoto wake. (Ukimtafsirie Mwingereza 'mother of so and so' msikilisaji ataweza kuchanganikiwa sababu gani kumwita na jina la mtoto wake?) Tena, maana yanapotea kwa ukalimani.

Ninawahaka ninavyo fikiri juu ya jinsi watoto WaAfrika wanavyo elimishwa na lugha geni kama Kiingereza, nikifikiria juu ya mambo aina hiyo ya hapa juu. Mimi ninadani kufahamu mambo yo yote ya ndani kwa masomo yao lazima kiwe kigumu. Ninashtuka pia ninavyoenda kutembea Ulaya - kukuta mashule ambayo yanafunza mambo yanayoenda (kwa ujumla) sambamba na maisha ya wanafunzi walioko. Kuenda shuleni ni kama mwongezo kwa mambo ya kawaida - na siyo mstuko ambao unampoteza au changanya mtu yanapogongana na hekima ya nyumbani.

Mwanafunzi anayetamani kuenda mbele hawezi kujali sana ikiwa mambo anayofunzwa hayalingani na mazoezi ya maisha yake, ikiwa itampa cheti ambacho baadaye kitamsaidia

7

Document info
Document views65
Page views66
Page last viewedWed Jan 18 15:47:26 UTC 2017
Pages9
Paragraphs145
Words4238

Comments