X hits on this document

311 views

0 shares

0 downloads

0 comments

13 / 50

follow. Haya, Kiswahili, Kijaluo. Ana kiki mago te, abiro temo kaka anyalo.

Kwanza nataka kuwajulisha staff yangu nilio nao. Nimekuja na wafanyikazi wawili kutoka kwa Commission upande wa secretariat. Hapa, Vivian hebu simama? Huyo mnaona huyu ni Vivian anatufanyia kazi katika Commisison lakini ametoka huko mbali Ukambani, Kang’undo. Mnataka awasalimie na Kikamba?

Audience: Ndiyo. Com. Pastor Ayonga: Vivian salimia hawa watu na Kikamba, hawa watu hawajasikia Kikamba na wao wasikie Wakamba wakisalimu watu wanasalimu namna gani. Salimia wao kwa Kikamba tu, watasikia.

Vivian Muli: Ovo wenyu (Laughter)

Com. Pastor Ayonga: Ndio, si leo mmepata salamu ya Kikamba?

Audience: Eeh.

Com. Pastor Ayonga: Huyu Vivian anatufanyia kazi katika ofisi na katika wakati huu ambao tuko hapa nje kazi yake utaona akitembea na hii kitu. Hii kitu mlikiona wakati wa kuchukua views? Hii kitu hatujawachana nayo, hii kitu kinashika maneno yako na kinashika maneno yangu na kwa hivyo, hata ule wimbo ambayo wale waimbaji wametuimbia hapa wa Katiba, ule wimbo umeingia hapa. Ni wimbo mzuri na wimbo ambao nimeona mtungi leo for the first time, nimeona jinsi mtungi inatumika, nimeona tena vitu vingine kule vijana wamechanganya vizuri na nikaona imechemsha na ndio imetuitia hawa watu. Kwa hivyo nyinyi waimbaji nawashukuru sana, nimewashukuru sana kwa wimbo wenu na tena mtakuja mtuimbie tena wimbo moja ambayo tutaweka hapa. Nitauliza kila mtu anyamaze, ili wimbo tu inaswe.

Halafu huyu kazi inakuwa ya kunasa maneno. Mwingine kule, hebu simama nyar Kisii. Simama, nataka wewe pia usalime hawa watu wetu hapa na Kikisii, mimi nawasalimia kwa Kijaluo, Vivian amewasalimia kwa Kikamba na wewe, huyu ni Mkisii kutoka Nyaribari…

Speaker: Nyaribari Chache.

Com. Pastor Ayonga: Ndio Nyaribari Chache umesema vizuri, ni kweli. Yeye ni lawyer by profession. Munene ni otin ni, to en a lawyer, ka ng’ato otimo na gimoro ka to ondiko case, case odonjo tayari. Hata nilisikia hapa ule wimbo wa Katiba unasema sasa akina mama ndio mbele. Na tena nikasikia wakisema chuon nindo, oooh. (Laughter) Chou muamke, nasikia nyinyi mnalala tu hapa upande wenu, eeh. Lakini wimbo imesema kwamba chuo nindo akina mama ndiyo mbele. Wacha hata wao wakitangualia bora tupate ugali na akirudi jioni atengeneze samaki vizuri, ile magira alete watu wakule. Sisi

13

Document info
Document views311
Page views312
Page last viewedMon Jan 16 13:26:27 UTC 2017
Pages50
Paragraphs810
Words17365

Comments