X hits on this document

349 views

0 shares

0 downloads

0 comments

16 / 50

kamani e kaka newa duaro.

Katiba ifanye kazi, hii ndio ifanye kazi, hiyo itakuwa maneno rahisi, wapitishe. Lakini hawa watu wanaweza kuja halafu wakiangalia ndio hii iko namna hii, hapa sisi hatutaki. Kama hutaki unatakaje? Tunataka hii mstari huu ubasilishwe. Kama unabadilishwa tusema nini? Tunataka usema hivi na hivi au hii itolewe kabisa, hii bado haijakuwa vizuri. Unajua mawazo ambao tumeweka hapa ni ya Wakenya wote, si mawazo ya Nyatike peke yake, ni mawazo ya Wakenya wote na utakuja kupata huko watapambana.

Mtu kutoka Coast atakuja kusema hapana, hii haiwezi kuwa namna hii, na wa Nyatike anasema sasa hii itakuwa namna hii, hapa hatubadilishi. Watu wawili wakipigana, si wanataka mtu watatu, eh? Kwa hivyo hawa watu wakishindana kuna maneno mengine wanaweza kusema tubadilishe hii na wakubaliane. Tutabadilisha hapo tu, wakikubaliana kwamba hii tuigeuze iwe namna hii, hiyo tutafanya namna hiyo lakini ikiwa watakuenda wasikubaliane na unaona wame split, basi sisi tunasema wakati huo jibu itatoka kwa nani, kwa wale waliotuambia hii. Go back to the people na wale people ni nani? Ni nyinyi ndio mtaamua na hiyo inaitwa, tunakuja kwa referendum.

Ikiwa ni referendum hiyo ni kazi ngumu, hiyo sasa tunaanza kusema watu wale wa election, Electoral Commission to take over, enda kwa watu waulize watu, hii maneno ni hivi na hivi, wewe unatakaje? Mimi nasema no, na wewe unatakaje, mimi nasema yes. Na yes’s zitahesabiwa na no’s pia zitahesabiwa for every change that is going to take place na ile itakayokuwa nyingi ndio tunasema watu wamesema hivi. Hii section itakuwa jinsi hawa wanavyosema na hiyo itachelewesha mambo. Tunatumaini kwamba watakapokuja huko hata kama wanaweza kufanya mabadiliko itakuwa tu si mabadiliko ngumu ile ambayo itahitaji nyinyi kuamua lakini itakuwa mabadiliko yale ambao yatakuwa madogo madogo.

Lakini sheria inasema watu ndio mwisho wa kila jambo, kwa hivyo nyinyi ni very important. Nyinyi ni very important kwa maana nyinyi ndio mmefanya hii iwe jinsi ilivyo na tunawashukuru kwamba kutoka mwanzo mlikuwa mnakuja wengi kutoa maoni yenu na maoni yenu tumeshaandika na sasa leo nimekuja ku-launch document hii. Hii document kama ingalikuwa vizuri ni kitu ambacho kingekuwa mmekipata sometimes back mkisome mimi nikija hapa mtaniambia kwamba upande huu tungalipenda iongezwe namna hii na tu-record hiyo tuende nayo. Lakini kwa maana hivi vitu hamkupata mimi leo kazi ambayo nitafanya ni ya kuwaeleza juu juu, kuwaambia hii iko, hii haipo, hii ipo, hii ipo, hiyo iko hapa ndani na kama mwishowe nikimaliza unaweza kuwa na wazo fulani tofauti basi unaweza kuongeza.

Leo si siku ya kuchukua maoni, la, si ile siku ya juzi. Leo ni siku ambao ninataka kuwaambia juu ya hii document, yale maneno mlituambia halafu nikishawaambia nitakuja kuwagawia haya magazetti ambayo ni draft Constitution na nitafuata register ile jinsi mlivyo-register na ninaona pengine hazitawatosho na ikiwa yoyote atakuja pungukiwa sasa mtapata copies zingine kutoka kwa Coordinator lakini hizi ni zangu ambazo nitawapatia hapa kwa maana siwezi kutembea bure. Kwa hivyo nitawagawia hizi, tumeelewana?

16

Document info
Document views349
Page views350
Page last viewedMon Jan 23 11:10:04 UTC 2017
Pages50
Paragraphs810
Words17365

Comments