X hits on this document

337 views

0 shares

0 downloads

0 comments

17 / 50

Audience: Sawa?

Com. Pastor Ayonga: Sawa kuna wangapi walikuwa wameshapata hiki? Hebu inua mkono juu, wale ambao mlishapata hii draft. Naoni ni hawa wachache wako hapa mbele yangu nyinyi wengine hamjapata, si hivyo?

Audience: La

Com. Pastor Ayonga: Basi kwa hivyo sitaki kutoa wakati huu, kwanza nitawaeleza ndipo nitaaanza kuwapa ili muende kusoma na mtakaposoma, kama kuna jambo ambalo linauzito kuna nani? Unaona huyu mama hapa, mtampa mawaza kwamba hii tunataka hivi na hivi halafu mwambie Mjumbe wenu wa hapa. Mjumbe hii tunataka hivi na hivi, basi na hiyo italetwa katika National Constitutional Conference. Nanaweza kuanza kwa kuwaelezea?

Audience: Ndio.

Com. Pastor Ayonga: Sasa wale ambao mmesimama si mtachoka.

Speaker: Endelea tu.

Com. Pastor Ayonga: Mimi niendelee, mkichoka si hata mimi pia nitakuwa nimechoka nitataka niketi chini. Sawa.

Sasa hii draft Constitution tulipokuja kwenu, kwanza hii draft ina chapters ishirini na chapter moja inatosha kama ningekuwa nazungumzia Pastor word by word niendelea itachukua kipindi mzima na mimi sitatumia hiyo. Nitawaambia yale juu juu, maneno makubwa juu juu halafu details, yale maneno mengine mtayapata ndani.

Katika hii draft Constitution, tulipokuja hapa kuchukua maoni mlituambia hii Katiba ya kwanza haina preamble. Nyinyi watu wa Nyatike mlisema hivyo? Kitu hicho mimi naita preamble, haina utangulizi, haina mwelekeo inaonyesha Wakenya tunaelekea wapi? Halafu tukawauliza hebu mtupe samples, mfano ya preamble. Tutakusanya preamble nyingi Kenya mzima na tukapata preamble. Ukienda uko ofisi yetu ma preamble yamejaa, yamejaa, yamejaa. Ukiandika preamble tu peke yake itakuwa kubwa namna hii na nani atabeba na nani atasoma. Kwa hivyo sisi tukaanza kuona, kwa jumla Wakenya wanataka nini na tukaandika preamble, tukasema Wakenya wamesema wanataka preamble na preamble hiyo tukaiweka katika utangulizi wetu. Kwa hivyo kuna preamble na hiyo preamble utakuja kuipata katika hiki kijitabu ambacho nitatoa baadaye na utaona kuhusu hiyo preamble. Wakenya wanataka hii, wanafikiri hivi, these are the expressions of the people of Kenya.

Ndipo katika hiyo preamble baadaye katika chapter ya kwanza mlituambia tuseme ni nani mkubwa hapa Kenya. Mkasema sisi

17

Document info
Document views337
Page views338
Page last viewedSat Jan 21 02:22:34 UTC 2017
Pages50
Paragraphs810
Words17365

Comments