X hits on this document

316 views

0 shares

0 downloads

0 comments

19 / 50

Com. Pastor Ayonga: Amevunja sheria, mnaona nchi zingine zimekuwa zikibadilisha capitals zao, leo ni hii orucha ni ile, oru machiel ni ile ingine. Sasa hii imekuwa kitu ambayo mwingine akiingia kwa power anaweza kubadilisha. Wazee mlipoenda shuleni na ile geografia mliosoma huko kwa Primary School, capital ya Nigeria ilikuwa inaitwa nini? Lagos lakini leo capital ya Nigeria iko wapi? Abuja. Hata ukusema Abuja haingii kwa kichwa yetu sisi old timers kwa maana sisi inakuja automatic, computer yetu ina-read Lagos na hii ya kuingiza ya dot.com hii inakwenda Abuja. Tanzania ua Tanganyika tulijua capital yake ni wapi? Dar es salaam. Lakini wakatu huu…

Audience: Dodoma.

Com. Pastor Ayonga: Dodoma hata wanafunze wengine hawaweze kujua hiyo wataanza kufikiri. Hata nilisikia mtu mwingine akiniambia ni Arusha, unaona? Kwa maana kitu ikiwekwa sawa sawa mambo inakuwa sawa sawa, kwa hivyo na sisi tumefanya yale mliotuambia. Ndipo mkatuambia habari ya lugha, kwamba lugha ya Kenya hapa ni lugha gani? Tukawauliza mkatuambia mnataka lugha ambazo zitatumika hapa Kenya, national language iwe Kiswahili, hii mlikubali?

Audience: Ndiyo

Com. Pastor Ayonga: Halafu mkatuambia official languages ambazo zitatumika zitakuwa Kiswahili na …? Audience: Kiengereza.

Com. Pastor Ayonga: Halafu tena mkatuambia, tunaona watoto wetu wadogo wanapotea, wanapoteaje, mtoto Mjaluo siku hizi unaongea naye Kijaluo hasikii, eh! Kwa maana anafundishwa lugha zingine za kigeni na mtoto anasahau yeye ni Mjaluo, lazima mtoto ajue kwanza yeye ni nani? Ni Mjaluo halafu asome hiyo Kiswahili, halafu hiyo Kingereza na sisi tukasema vernacular languages wakati ambapo mtaenda kusoma, utakapoangalia sehemu ya culture, utamaduni ya watu utakuja kuona tumazungumzia juu ya languages, venacular languages. Kwa hivyo, hiyo pia iko ndipo vitu vingine ambavyo mlituambia….(End of tape A, side A)

Mipaka ya dini na mnataka akuona mipaka ya serikali na tukawauliza, mnatuambia hii ni nini mnasema. Tunasema kwamba dini ikichanganywa na serikali italeta madhara kwa watu kwa maana mmeona sehemu zingine ambapo dini na serikali hakuna tofauti.

Kwa mfano mnaona shida iko Sudan, Waislamu na Wakristo. Ile inakuja kwa maana serikali inakuwa ya Kiislamu na kwa hivyo Mkristo akiwemo anaambiwa yeye ni adui, yeye hafuati serikali. Kwa hivyo sisi tumeweka dini na serikali as separate, mtua abudu jinsi anavyotaka kuabudu, serikali itawale watu wote bila kutumia dini katika utawala. Kwa hivyo tuliweka hivyo jinsi mlivyotuambia.

Ndipo tena mkatuambia National symbols, alama zitakazotumika kwa mfano, mmeshatuambia habari juu ya pesa. Hii pesa sasa kila President akija atawekwa, kila anayekuja atawekwa au tungefanya namna gani na hiyo watapigana huko Nairobi

19

Document info
Document views316
Page views317
Page last viewedTue Jan 17 03:16:39 UTC 2017
Pages50
Paragraphs810
Words17365

Comments