X hits on this document

325 views

0 shares

0 downloads

0 comments

20 / 50

watakapokuja. Kwa maana mmetuambia mnataka mifana inayowekwa isiwe ya mtu, inaweza kuwa pengine kitu kimewekwa kama Lake Victoria ambayo ni bahari au mlima fulani au kitu fulani cha Kenya inaweza kuwa ni samaki, inaweza kuwa ni mahindi, inaweza kuwa ni chai. Kitu kinachoweza kuwekwa ambacho si cha mtu lakini cha watu wote na kwa hivyo hiyo iko subject kwa kubadilisha hii au ile, ni ipi itakayopendwa lakini mawazo ya watu ni kwamba tuwache kutumia vichwa vya watu.

Audience: Sawa sawa.

Com. Pastor Ayonga: Mambo mengine mliotuambia ni habari ya holidays pia. Mlisema sasa holidays zinazidi kuwa nyingi sasa kila mtu akija naye atawekewa holiday yake na miaka jinsi inavyoelekea itakuja kuwa kwamba holidays za watu zimekuwa nyingi. Kwa hivyo tuchukue tu National days ambazo ni za holiday. Kitu kama Christmas ambayo uwezi kutoa, kitu kama siku ya Jamhuru, kitu kama siku tulipopata uhuru na mambo mengine. Wengine mkatuambia hivi au vile hayo yote tumeshaweka katika hii draft. Halafu mmetuambia habari juu ya raia, citizenship. Hii mliongea, mkaongea, mkatuambia watoto wetu wameoa huko nje wakija mtoto amekuja na Mzungu, huyu anasumbuliwa hapewi uraia wa Kenya na mtoto wetu ameolewa nje akija na huyo mgeni na wanataka kuishi kama Wakenya haya mambo tuyaangalie. Hayo yote tumezungumza jinsi mlivyotaka, jinsi Wakenya walivyotaka na tumeyaweka na utayasoma hapa katika hii draft.

Kwa hivyo, tumeweka sheria ikiwa mtu ametoka hivi, huyo atachukua muda huu ndipo aweze ameangaliwa mwenendo wake, amejua lugha yetu, amejulikana mguu yake haikukanyaga huku na kule. Mkatuambia juu ya uraia wa namna mbile, ule mnaita dual citizenship. Mtoto watu ameenda kusoma ng’ambo, ameenda huko akawa mwa Amerika na akija hapa Kenya Ukenya wake utakuwa namna gani. Hayo yote tume-deal nazo, tumesema Mkenya ni Mkenya awe amekanyaga ng’ambo au awe amekanyaga hapa, hapo ndio kwao hawezi kunyimwa uraia wake wa nyumbani. Ule mwingine anaweza kunyang’anywa lakini huyu wa kuzaliwa wa baba yake ambaye ametoka pahali fulani hiyo bado atarudishiwa na ataendelea nayo.

Kwa hivyo tumefanya hayo mambo yote juu citizenship ndipo tumeenda pahali pengine ambapo mlituambia mnataka kujua ile bill of rights. Haki za binadamu, misingi ya haki na uhuru wa watu na tukasema ni sharti serikali iangalie, kuongeza na kuweka mkaza juu ya haki za watu. Mtu ana haki ya kuishi, una haki ni mtu na ni lazima uishi, ni lazima utunzwe na ni lazima Chifu akupe security. Chifu, hawa watu wako wote lazima wapate security.

Joseph Omoyo (Chief): Kutoka kwangu.

Com. Pastor Ayonga: Kutoka kwako, hakuna mtu atakayenyanyaswa kwa maana kuna sheria na mkatuambia lazima tuwe equal, tuwe sawa sawa. Usawa, yule kama ni ngane yeye atafanyiwa hivi na mwingine akija anaambiwa wewe hakuna kitu kama hiyo. Una haki ya kuweza kutendewa kama Mkenya mwingine yeyote, kila kitu ambacho kinachotakikana.

Una haki ya kutobaguliwa, usibague kwamba huyo ni fulani wa huko hatujali, huyo ni fulani wa huko hatujali, la kila mtu yuko

20

Document info
Document views325
Page views326
Page last viewedWed Jan 18 20:56:31 UTC 2017
Pages50
Paragraphs810
Words17365

Comments