X hits on this document

350 views

0 shares

0 downloads

0 comments

22 / 50

Kwa maana hawa watu wawili wasipoishi vizuri matunda tutakayopata au mazao yatakuwa mabaya, kwa hivyo lazima tuangalie habari ya watoto, tuangalie habari ya family. Tuangalie habari ya masilahi ya disabled, wale watu ambao ni walemavu, watu wasiojiweza kwa njia moja au ingine. Tumechukua chapter ambayo inaendelea kuonyesha walemavu wafanyiwa hivi, wawe na equal rights kwa hivi na vile na wao watendewe haya na yale bila ubaguzi.

Halafu tuna freedom of religion, belief and opinion. Kila mtu anahaki ya kuchagua dini ambayo anaweza kufuata au kufuata mambo ambayo ameamini bila ya kuingiliwa na mwingine na hayo ni mambo ambayo yalio ya muhimu. Mtu asilazimishwe kuwa hivi au vile lakini mwenyewe haruhusiwi kufanya ni nini anataka kufanya katika beliefs zake.

Halafu tuna habari juu ya property, ownership of property. Una haki ya ku-own property ambayo inaitwa yake. Mwanamke ana haki ya ku-own property ambayo inaitwa yake na hawezi kuzuiliwa, hiyo ni mojawapo ya those rights ambazo zinatakikana mtu kuwa nayo.

Habari ya afya: Uko na haki ya kupata madawa, unahaki ya kugangwa ukiwa mgonjwa kawa maana tulipokuja kwenu hapa mlituambia oh, dispensaries, mahosiptali siku ukienda hakuna dawa. Ni jukumu la serikali kuona kwamba they care for the health of their people. Kwa hivyo un haki ukiugua ugangwe. Una haki ya kuwa na afya nzuri, ya kuwa na mazingara mazuri, haki ya kula, haki ya kuwa na maji safi na utunzaji wa mazingara yetu, environment.

Ndipo tutakuja kupata tumeandika juu ya electoral system. Mlituambia kwamba mnataka wakati huu katika Katiba yetu mpya kwamba watu wanapochaguliwa, kura zinapopigwa kura hizi zihesabiwa hapo hapo. Si mlisema hayo maneno.

Audience: Ndio.

Com. Pastor Ayonga: Na tumesema katika Katiba yetu mpya ikiwa watakubali kwamba kama kura zilikuwa zimepigwa hapa, kama mlolongo ilikuwa inafanywa hapa ya kuweka kura katika debe, baada ya watu kwisha zihesabiwa hapo hapo watu wakiona na isemekane ng’ane umepata 200, huyu akapata mia saba, huyu akapata nini katika polling station ili kila mtu akitoka ametosheka. Kwa maana kama inapelekwa Migori, ikifika kona kona zenu hizi ambazo nimeona ingine itaongezeka, ingine itapotea na mambo yanaenda yakawa namna ngumu. Kwa hivyo hata kazi ya kuhesabu kura inakuwa rahisi kama inafanywa hapa mbele ya watu, sasa ni number 2 ndio inayotumwa na number ikienda kuongezwa hata na wewe unajua ilikuwa hipi.

Halafu mkatuambia pia, watu ambao mnataka waende Bunge mnataka watu ambao wamesoma na sasa tukaenda tukapata Kenya nzima inasema mtu akienda Bunge lazima awe ana degree na sisi tukasema hivi. Mlisema kwa hivyo tumeandika hiyo mtasoma. Halafu mkatuambia Bunge iwe na nyumba mbili, Upper na Lower House na sisi tumeweka hiyo na utakaposoma utaona hawa watafanya nini na nini.

22

Document info
Document views350
Page views351
Page last viewedMon Jan 23 14:53:52 UTC 2017
Pages50
Paragraphs810
Words17365

Comments