X hits on this document

334 views

0 shares

0 downloads

0 comments

23 / 50

Tukaenda pahali pengine, ninapoguza Bunge nimeingia Parliament. Mkasema kwamba mnataka hawa watu wa Parliament wawe Wabunge tu, wakienda huko wao wawe watchdogs wa kuangalia kule kunafanyika nini, kule kunafanyika nini na wawe wanahusikana na mambo ya Bunge tu. Mkatumbia wasiwe Ministers, ikiwa hapa kwenu hamkusema tumeambiwa Kenya mzima na tukauliza mnatakaje, mkasema mmeanza kuona Ministers ambao wamewekwa katika Ministries ambazo hatajuhi what is going on. Mkatuambia mnataka Ministries kuongozwa na professionals, basi tukasema kila ambacho mmesema ndicho hicho tumesema, tunajua hiyo joto itakuja kutokea watakapo pambana lakini sisi tumeweka mawazo yenu.

Halafu mkatuambia katika uchaguzi mnataka President achaguliwe na watu wote na President asiwe na constituency, tukasema President ambaye atakuwa constituency yake itakuwa Kenya. Kenya mzima ndio constituency yake lakini hana constituency yake kama President alikuwa anatoka Nyatike tena hapa yeye ndiye MP wa Nyatike, hapana. Tunataka huyo mtu anatoka Nyatike awe yeye Kenya nzima ndiyo Nyatika yake halafu mkatuambia hamtaki Vice President ambaye anachaguliwa na President ndipo tukasema basi huyu Vice President yeye atakuwa a running mate ya President wakati ule wa kuchaguliwa. Basi atakuwa mtu ambaye naye amechaguliwa na watu na kwa maana amechaguliwa na Watu President hana uwezo wa kutoa huyu.

Speaker: Sawa.

Com. Pastor Ayonga: Mkasema hamtaki hii radio ya saba unasikia fulani ameangukia pahali fulani. (Laughter) Mkasema mnataka Vice President ambaye ataendelea na yeye na ku-define kazi yake, anajua yeye ni Vice President. President akienda ng’ambo ile yeye kama yuko ng’amo hii anatawala kwa hivyo asije akawa yeye ni mfanyikazi wa huyu. Awe ni Vice President ambaye anafanya kazi ya Kenya mzima, basi hiyo tukaweka.

Na mkatuambia mnataka Prime Minister na Prime Minister mkasema achaguliwa kutoka Parliament na kile chama ambacho kina watu wengu na huyu ndiye awe leader of the government business. A-run serikali from day to day work, hiyo ndio kazi ya Prime Minister na huyu Prime Minister awe na ma-Deputy wangapi?

Audience: Wawili.

Com. Pastor Ayonga: Wawili, hiyo tumeweka mtakuja kusoma hapo muone kazi ambayo atakuwa anafanya. Kitu gani ingine mlituambia?

Mkatuambia kuamba Parliament iwe na uwezo au hata kwanza kabla hatujaenda katika uwezo mkasema nyinyi mnatakiwa muwe na uwezo. Kwamba mkituma mtu Parliament na huyu mtu alikuwa ameenda huko amewaambia maneno matamu matamu hapa mkafikiri ataweza na akienda huko mkapata hafanyi chochote. Kwamba tuwape power of recall, ya kuweza

23

Document info
Document views334
Page views335
Page last viewedFri Jan 20 07:53:26 UTC 2017
Pages50
Paragraphs810
Words17365

Comments