X hits on this document

323 views

0 shares

0 downloads

0 comments

24 / 50

kusema turudishiwa, back to the sender.

Audience: Sawa. (Applause)

Com. Pastor Ayonga: Na sisi tukasema wananchi wa Kenya wamesema kama a non performing Member of Parliament ameonekana kwamba wananchi wanaweza kusema rudisha na tutachagua mwingine. (Applause)

Halafu mkatuambia hizi three arms of the government, Executive, Parliament na Judiciary kwamba ziwe truly independent. Kwamba mnaona jambo likifanywa huko na executive litaenda likageuza mtu hapa na ataitikia sauti ya huyo. Mkatuambia koti mnaona hazifanya kazi viziru kwamba corruption imejaa na corridors zake hazina harufu nzuri zina mambo mabaya mabaya huko na mkasema mnataka tuangalie maneno ya koti. Na sisi tulipoenda kuangalia sasa mnaona tuliguza nyuki, tukaguza nyuki mpaka nyuki inapiga sisi, inasema tupelekwe kotini na sisi ndio maana yake tuko hapa tukikimbia tunaendeshana hatujaenda kotini. Wao wanatukimbiza sisi kotini na sisi tukohapa tunaweka yellow ribbon, bendera yetu, tunaweka kwamba sisi kazi tuliopewa tunatumikia wananchi na wao waendelee kujenga jela kubwa nyinyi nyote mtakuja kuchukuliwa kwa maana maneno sisi tulioandika ni maneno yenu.

Kwa hivyo mkasema mnataka these three Arms of the government ziwe independent na mkazema tupunguze uwezo au kazi za President na pia hapo tukapunguza. Tukasema ndio maana yake tuliweka Vice President ambaye anaweza kufanya kazi, ndio maana yake tuliweka Prime Minister ambaye anaweza kuendesha mambo ya day today running of the government. Kwa hivyo hawa watu wakiwa-independent, tukasema President anaweza ku-appoint mtu lakini awe vetted na Parliament. Parliament inaweza kukataa, hapana huyu hawezekani lete jina lingine, lete jina lingine huyu haiwezekani na kwa maana mtu wa hakuandikwa na President huyo mtu atakuja kuja kuwa independent ka kazi anayofanya. Kama fulani amesemwa atakuwa Judge wacha CV yake iende kwa Parliament, Parliament iangalie kweli, what is the past performance ya huyu mtu. Amefanya hivi na hivi, huyu amefanya hivi na hivi, ndio we agree huyu mtu ataweza. Kwa hivyo huyu mtu atakuwa anafanya kazi kwa maana anaaminika kwa hivyo, vetting imekuwa jambo la maana sana.

Ndipo, maneno ni mengi niliwaambia nitaguza kidogo kidogo. Ndipo tukasema Parliament ijifanyie programme yake, ni wakati gani itafungwa, ni wakati gani ita-sit, ni wakati gani itakwishi? Hayo maneno, ili hata mwananchi yoyote awe anajua, isiwe ni siri, hakuna kitu cha siri. Tuwe tunajua kwamba hata uchaguzi ukija unakuja mwaka fulani, mwezi fulani, tarehe fulani, hiyo itafanywa kwa hivyo hayo yote tumeweka na hata tumesema ni lini ingekuwa inafanywa. Na mkatuambia kwamba mnataka President awe kwa miaka kumi ya vipindi vya miaka mitano mitano, kwa hivyo hiyo tuliweka.

Tukaingilia maneno ya natural resources: Mlituambia mnaona vitu vingi ambavyo watu wanavyo katika sehemu yao, katika Country Council yao, katika district yao. Unapata viti hivi vinaweza kutolewa hapa na vikatumika pahali pengine bila ya hawa watu kupata kitu. Kwa hivyo mkasema mnataka kuona vitu ambavyo mko navyo na nyinyi mnafaidika na hivyo vitu, visiwe ni

24

Document info
Document views323
Page views324
Page last viewedWed Jan 18 12:09:58 UTC 2017
Pages50
Paragraphs810
Words17365

Comments