X hits on this document

321 views

0 shares

0 downloads

0 comments

25 / 50

mwingine ndiye anavyevitumia na nyinyi hamvitumii. Kwa hivyo mkataka hivi vitu muweze kufaidika kutoka kuwa na vile vitu na kulinda natural resources, County Council jinsi ambavyo inaweza kulinda vitu hivi ili County ile iweze kufaidika. Kama ni maji au ni electricity au ni misitu, vitu hivi viweze kufaidisha watu wa upande ule.

Pia mkatuambia mnataka Provincial Administration itolewe, hiyo bado ingali inapingwa lakini mlituambia na sisi tumeweka. Provincial Administration, Chifu wanasema mtolewe wewe ng’oja tu. Wanasema kwamba Provincial Administration tulionayo ni relic ya mkoloni lakini tena na wengine wakaenda wakauliza, sasa kama kutakuwa hakuna Chifu na mwingine aliiba kuku yangu hapa tutafanyaje? Ndipo mkatuambia, tunataka watu ambao wanafanya mambo hayo wawe wanachaguliwa na sisi. Mkasema DC aende sisi tutachagua mtu wetu, eh! DO aende, sisi tutachagua mtu wetu na Chifu, tutachagua mtu wetu si mtu wa kuwekelewa na hawa watu watapewa tu majina tofauti ila kazi ambazo watafanya ni ile. Na mkasema mzee wa kijiji alipwe mishahara, eeh!

Audience: Sawa. (Applause)

Com. Pastor Ayonga: Kwamba hawa wazee ndio wanafanya kazi nyingi sana, kwa maana wao ndio wana-settle cases za jamii na mkasema pia mnataka mambo mengi ya kinyumbani yafanywe kinyumbani yasipelekwa High Court kwa maana nyinyi ndio mnayajua hayo mambo. Mkasema title deeds ziwe zinapatika hapa karibu usiende huko mbali hata mtu anaenda akauza shamba chake na akaenda akampa mwingine title deed ambayo haijulikani. Wazee wa kijiji ndio wa-settle, ndio wanajua hapa ni kwa fulani, tong’ yake iko kule na kweli hii shamba ilikuwa ya mzee fulani na inauzwa sawa sawa. Sasa kuna mashamba mengi unauziwa kumbe ni shamba la mtu unauziwa na kwa maana unafanywa huko mbali hamwezi kujua fulani ana-title. Kwa hivyo mwenye title naye ataenda auziwe mwingine ampe pesa na mambo haya yameleta shida, kwa hivyo mlikuwa mnataka mambo yote yaletwe karibu na hiyo kuleta karibu tumeweka katika hii Katiba. Na nyinyi sasa musome pole pole, mtafune na msema hapa haijawekwa sawa sawa. Ka ok ayiego, hawa watu hapa waliweka hiyo lakini si hiyo mimi nilitaka hivi na hivi na hivi, kwa hivyo mnamwambia huyu mama.

Sasa mambo yote ambayo mlisema kwa ufupi yako hapa na tena mkasema, kabla sijaketi ili niwape nafasi. Mkasema mnataka hii Katiba iandikwe kwa lugha ambayo mnaweza kusoma. Ile ya zamani mkasema imeandikwa kwa lugha ngumu thelathini, maneno mengi yamejaa huko hata lawyers wengine hawaelewi, wanataka utoe pesa kwa fulani ndipo akueleze hiyo maana yake ni nini. Watu wanafungwa fungwa na huwezi kuelewa kwa maana clause hii, kumbe ina-mean kitu namna hivi na wewe unakwenda gikori ka iparo ni ing’eyo tiende lakini hukuelewa. Kwa hivyo tukasema, hii Katiba itaandikwa in a simple language ambayo ni straight forward, si ile ya kuenda kando kando, ya kutaka dictionary. Ni ile ya kusoma straight, hauelewi Katiba iko namna hii, inasema hivi. Nikifanya hivi nimepotea na iwekwa kwa lugha mbili, Kiingereza na Kiswahili.

Kwa hivyo hii Katiba itapatikana katika hizo lugha if it issued na mwingine aliniuliza. Commissioner sasa hiyo unasema hiyo kitu mimi naona wewe unabeba ni kubwa sasa hii kitu kubwa nani atakuja kubeba hii. Nikawammbia hivi, unataka hii Katiba

25

Document info
Document views321
Page views322
Page last viewedTue Jan 17 17:38:27 UTC 2017
Pages50
Paragraphs810
Words17365

Comments